Thursday 28 July 2011

ALI KIBA NA MADANSA WAKE WANUSURUKA KATIKA AJALI YA GARI




Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ali Kiba pamoja na madansa wake alfajiri ya(Jumapili) wamenusurika vifo kufuatia kupata ajali ya gari katika eneo la Mikumi mkoani Morogoro walipokuwa safarini kutokea Mbeya kuelekea jijini Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika gazeti la Nipashe ambazo BC imeweza kuzithibitisha kutoka kwa Ali Kiba mwenyewe,jumla ya watu saba wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya mkoa Morogoro.Ali Kiba ambaye aliumia mguuni na mkononi  tayari ameruhusiwa kutoka hospitali na amesharejea nyumbani kwake Dar ambapo ameieleza BC kwamba anaendelea vyema. Ali Kiba alikuwa awe miongoni mwa wasanii waliotumbuiza katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyikia CCM Kirumba Mwanza hapo jana.
Chanzo kamili cha ajali hiyo hakijawekwa wazi na polisi tayari wanachunguza.BC inawatakia wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo kupona haraka ili waweze kurejea katika kazi zao.


No comments:

Post a Comment