Thursday 28 July 2011

Mr.& Mrs.Gervas Mbwiga........




Endapo ulikuwa na “kajindoto” ka kuuteka moyo wa mtangazaji wa kituo cha Times FM(siku hizi wanasikika mtandaoni kupitia timesfm.com) anayekwenda kwa jina Hadija Shaibu au almaarufu kama Dida,itakubidi ndoto hizo uziweke kapuni japo kwa sasa.Kwanini?
Ni kwamba mapema hii leo,Dida amefunga ndoa kwa mujibu wa sheria(bomani) na Bwana mmoja anayekwenda kwa jina la Gervas Mbwiga jijini Dar-es-salaam.Hii ndio ile ndoa ambayo vyombo vya habari(zaidi magazeti “pendwa”) yaliripoti kwamba Dida mwenyewe hakuwa anajua full details za mpango huu!Kama wanavyoonekana pichani,ni wanandoa wapya wenye raha na uamuzi wao wa kuuaga ukapera.Tunawatakia kila la kheri.

Picha ya Global Publisherz


No comments:

Post a Comment