Thursday 30 June 2011

ISHA MASHAUZI KUMSINDIKIZA MKUBWA FELLA KATIKA MPAMBANO WA NANI MKALI KATIKA WASANII WA KIZAZI KIPYA CHA TAARAB 1st JULY-EQUITOR GRILL TEMEKE


Isha mashauzi
Mkubwa FELLA kiongozi wa kundi la bongo fleva TMK Family yakina Temba na Chegge, ambaye pia ni msanii chipukizi ktk Taarabu atachuana na wasanii wengine watatu chipukizi ktk miondoko hio ya muziki wa Taarabu ktk kumtafuta Mkali nani kati yao Ijumaa hii pale EQUATOR GRILL, Mtoni kwa Aziz Ally


Show hio ya aina yake itaanza mishale ya saa 2 usiku huku ikiongozwa na Kings Modern Taarab wanaotamba na nyimbo kibao kwasasa ikiwemo "Kijoka" na kusindikizwa na ISHA MASHAUZI mkali wa "Mama nipe Radhi" na zingine nyingi.









Wasanii wa kizazi kipya cha Taarab watakaopanda jukwaani kuoneshana nani mkali ni wale wanaotamba sana ktk medani hizo ambao ni Mkubwa Said Fella na nyimbo yake ya "Simuachi"aliyomshirikisha Isha, Athumani Ally "Nyongo mkalia ini"Omary Ally"Simuachi mpenzi wangu" na Kepteni Temba "Nimeiteka himaya".