Wednesday 29 June 2011

WEMA AMWANGUKIA KANUMBA

Wema Sepetu



Steven Kanumba

Wema, alimvaa Kanumba hivi karibuni mjini Dodoma, wote walipojumuika kwenye Klabu ya Bongo Movie kwenda kusukuma kabumbu na netiboli dhidi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo cha habari kinapasha kuwa wawili hao waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kutibuana, walifanya kikao Juni 19, 2011 (Jumapili) kwenye Hoteli ya African Dream, Dom ambacho kiliongozwa na gwiji wa maigizo Bongo, Jacob Steven ‘JB’.

Kilisema kuwa Wema aliona amepata mwanya wa kuzungumza na Kanumba, hivyo alimvaa na kumuomba JB awe msuluhishi kwa sababu anaamini kati yao bado kuna kinyongo.

“Wema alimwambia Kanumba mbele ya JB kuwa anaomba wasameheane, kinyongo kiishe,” kilisema chanzo chetu ambacho ni kati ya wasanii wanaounda Klabu ya Bongo Movie Netiboli.

Kiliongeza: “Wema alimsihi JB amwambie Kanumba aache chuki. Alidai mpaka leo Kanumba anamchukia na hataki hata kukaa naye wazungumze.”

Chanzo chetu kilisema kuwa pamoja na Wema kujieleza kwa kila namna, bado Kanumba aligoma na zaidi alikuwa akimjibu mrembo huyo: “Tuelewane nini mimi na wewe? Kila mtu anajua wewe sasa hivi ni mke wa Diamond. Unataka niwe na maelewano gani na wewe mke wa mtu?”

Kwa jibu hilo la Kanumba, chanzo chetu kilimkariri Wema akisema kwa unyonge: “Mimi ni mtu mbaya lakini ni vizuri nikapewa nafasi. Nahitaji tuondoe hizi tofauti tuishi kwa amani, kila mmoja aondoe kinyongo na mwenzake. Mimi sina chuki lakini wewe unaniona adui.”
Kwa mujibu wa chanzo chetu, JB alitumia busara kujaribu kuwafanya wamalize tofauti zake lakini Kanumba aliweka ngumu na kuahidi kuwa hatamsamehe Wema.

“Kikao kilivurugika baada ya watu kuwakuta wakizungumza. Ray (Vincent Kigosi) alishangaa sana kukuta Kanumba na Wema wanazungumza kwa sababu anajua ni maadui. Baada ya muda, JB aliondoka, kwa hiyo kikao kiliisha bila muafaka. Kanumba alibaki na msimamo wake kwamba hawezi kumsamehe Wema

No comments:

Post a Comment